send link to app

Twenzao


4.4 ( 144 ratings )
Viagens
Developer: Amos Mushumbusi
Livre

Umewahi kuwa unaendesha gari binafsi ukiwa na siti tupu ukatamani ungepata abiria wa kukuchangia gharama za mafuta?
Umewahi kuachwa na basi ukatamani ungeweza kupata usafiri wa gari binafsi kwa namna rahisi na kwa bei isiyozidi ya basi?

Jibu lako ni "Twenzao", app inayokuunganisha dereva wa gari binafsi na abiria wanaoenda mwelekeo wako. Hakuna makato yoyote kutumia app ya Twenzao, anacholipa abiria ndicho anachopata dereva.

Twenzao inakuhakikishia usalama wako, taarifa za wasafiri wote tunazo, wawe ni madereva au abiria, na pia app ya Twenzao inakusanya taarifa kuhusu safari yenu, kwa mfano mahali mlipo.

Faida za Twenzao kwa ufupi:
- Starehe ya gari binafsi kwa bei nafuu isiyozidi ya basi.
- Safiri salama na watu ambao taarifa zao zimehakikiwa na safari yenu inatambulika.
- Kwepa usumbufu wa madalali.
- Anza safari muda wowote, sio lazima alfajiri kama ilivyozoeleka.
- Pata safari hata kwenda kwenye vijiji ambapo mabasi hayasimami.
- Kuwa huru kusimama au kutosimama safarini kuendana na makubaliano yenu mnaosafiri.

Twenzao, safiri salama kwa bei nafuu.